Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) –ABNA– Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Masoud Pezeshkian, ameitoa shukrani za dhati kwa serikali na wananchi wa Iraq kwa mchango wao mkubwa katika kuandaa na kuhudumia shughuli za kuaga na kusafirisha mwili wa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei.
Katika ujumbe wake, Pezeshkian alisema kuwa wananchi wa Iran hawatasahau kamwe misimamo ya kindugu, mapokezi ya heshima na mandhari ya kugusa hisia yaliyojitokeza wakati wa shughuli hizo, ambazo alizieleza kuwa ni za kihistoria.
Rais huyo alisisitiza kuwa mshikamano ulioonyeshwa na serikali pamoja na wananchi wa Iraq umeimarisha zaidi uhusiano wa kidugu kati ya mataifa hayo mawili, huku akieleza kuwa kumbukumbu za mazishi hayo makubwa zitaendelea kubaki katika historia ya Iran na Iraq.

Your Comment